Hii mada nimeona niiandike haraka sana kwani tunakoelekea kubaya wanawake wenzangu, siku hizi eti wanawake ndiyo tunaongoza kufumaniwa aibu sana hii, tunaziaibisha familia zetu na  tulikotoka jamani.
 
Hivi ni kwa sababu gani wanawake  tumekosa haya na kuamua kushindana na wanaume, wakati mwingine ni hulka tu ya mtu, kwa nini usiache tabia zako huko kwenye ujana unataka uziingize mpaka kwenye ndoa, hivi mnajua maana ya ndoa lakini? Wenye tabia mbaya waseme kufumaniwa sasa basi.
 
Sasa niwaambie basi si wanaume wote wakiwa hawapo nyumbani wameenda kujiachia na wanawake wengine la hasha, mwanamke jiheshimu kulingana na heshima yako, mwanaume wako anavyotoka nje ya nyumba au mji anakuwa amekwenda kutafuta kwa ajili yenu.
 
Jaribu kumuonea huruma 
Kwa mwanamke mwenye mapenzi na mumewe anatakiwa kumuonea huruma mume wake hasa pale anapogundua amekwenda kufanya kazi kwa ajili ya kutafuta riziki ya familia, kwani anachotafuta ni kwa ajili familia nzima.
Mashosti, baadhi ya wanawake wana tabia mbaya, wamekuwa ni watu wa kuingiza wanaume ndani ya nyumba zao ambazo wanaishi na waume wao wa ndoa, hivi hujisikii vibaya kuingiza jasho la mwanaume mwingine kwa mume wako wa ndoa? Kwa nini unamuadhibu hivyo, amekosea nini?
 
Wengi wanaofanya hivyo ni wale ambao waume zao wanasafiri kwenda nje ya mji! 
Mwanamke mwenzangu ni kwa nini uwe na fikra mbaya kuwa mumeo lazima kila mkoa ana mke na wewe unaamua kujiingiza pabaya?  Huoni kufanya hivyo ni kuamua kuleta magonjwa ndani ya nyumba. Chunguzeni wanawake wengi siku hizi ndiyo sababu ya kuenea ugonjwa wa Ukimwi lakini wanaume zao hawajui ni mbaya sana mashosti tunatakiwa kubadilika, hali imekuwa mbaya.
 
Kama unahisi mumeo ana mtu fanya hivi
 Kama unahisi mumeo ana mwanamke kwa hisia tu, mchunguze na ukigundua ni kweli mketishe aache tabia hiyo lakini nawe jishughulishe na ujasiriamali kwanza, kwa kujichanganya na watu utasahau fikra potofu na utaweza kujiingizia kipato na siku zitaenda utashtukia mnakaa vyema na mumeo, kama alikuwa kiruka njia anarudi nyumbani.
 
Kwa kufanya hivyo familia yenu itakuwa yenye furaha na amani na kipato kitaongezeka kwa sababu wote mtakuwa mnajishugulisha.
 
Mume akisafiri fanya haya 
Siku ya kusafiri mumeo hakikisha unakaa naye chini kwa lugha ya upendo, unamuomba awe mwaminifu aendako kisha unamuombea dua asafiri salama kwani huko atakutana na mengi.
Kuna ajali za barabarani na misukosuko yote unayoijua kwa safari, sasa kwa dua na mashetani yanayopita yatapita mbali kabisa hata kama anawaza kukusaliti atashindwa kwani akikumbuka jinsi mlivyoagana roho itamsuta.
Jenga tabia ya kumuuliza amefika wapi na kumtakia safari njema awapo njiani.
 
Akikaribia kurejea nyumbani ufanye nini? 
Siku ukiona mumeo anakaribia kurudi hakikisha unafanya usafi wa mwili wako pasipo kawaida kama hupendezi basi pendeza kwa ajili ya kumpokea mume, muandalie chakula kizuri na uhakikishe unampikia kile roho inapenda.
 
Kabla ya kufunga mada hii nasisitiza wanawake wenzangu ni aibu sana kufumaniwa acheni mambo ya mafiga matatu ni mabaya na mwisho hayana faida yoyote kwani utapata aibu na ugonjwa je, familia utamuachia nani...??

Comments