Wema Sepetu amekanusha kurudiana na mpenzi wake wa zamani Chaz Baba japo amedai kuwa muimbaji huyo wa muziki wa dansi ndiye mwanaume wa pekee ambaye hakuwa na masuala ya kiswazi baada ya kuachana.
 
Wema ameiambia U Heard ya Clouds FM Jumatano hii kuwa Chaz Baba kwa sasa ni mshkaji wake na hata alipooa alimchangia pesa.
 
“Chaz Baba alikuwa ni mshikaji wangu naweza kusema ndio boyfriend pekee asiye na mambo ya Kiswahili,” amesema. “Tulizinguana tukafika pointi tukasaidiana, ameoa nikamtolea mchango, nimeenda kwenye harusi yake sioni tatizo.”
 
“Mimi na Chaz Baba tulikuwa tunapendana na baada ya kufikia point ya kuachana tukaachana, tukawa hatuongei for sometime mwisho wa siku baada ya kila mmoja kukaa kwake tukawa tunazungumza. Sio kama watu wengine tukigombanaga tunatafuta mabifu, hatusemeshani,” ameongeza mrembo huyo aliyesisitiza kuwa ‘sina bwana’.

Comments