Kampuni ya teknolojia ya Google jana imetangaza mpango wake wa kuanza kutengeneza magari yatakayokuwa yakijiendesha yenyewe bila dereva. Magari hayo yanatarajiwa kuanza kuingia barabarani ndani ya mwaka mmoja.

google car1

Muasisi wa kampuni hiyo Sergey Brin alizindua gari hilo la kipekee katika mkutano na wanahabari huko California na kuongeza kuwa lengo lao la kutengeneza magari hayo ni kuwapunguzia watu kazi ya kuendesha gari.

google car2

Brin ameongeza kuwa magari hayo hayatakuwa na usukani, pedal ya breki wala accelerator badala yake yatakuwa na kitufe cha ‘Stop-Go’ pamoja na screen inayoonesha njia inapopita. Software pamoja na sensor za Google ndio zitamaliza kazi yote iliyobaki.

Magari hayo yatakuwa na mwendo wa 25mph.

Comments