Na Gerald Kitalima
Mwanamuziki nguli wa kike hapa Tanzania Lady Jaydee ambae kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa Forever amefunguka na kuonyesha kukerwa na kitendo cha
baadhi ya mashabiki wake wa Instgram ambao walimuelewa vibaya baada ya kupost picha jana na kusema kuwa tumbo lake limevimba baada ya kupata msosi wa maana na mzuri,Mashabiki hao wengi wao walitafsiri kuwa Mwanadada huyo kwa sasa ni Mjamzito baada ya kuona picha ile na maneno ya Jide yaliyosomeka kama Tumbo limevimba sababu ya sahani.
 
Lady Jaydee alibidi aifute ile post aliyopost na kupokelewa tofauti na baadhi ya mashabiki wake na kisha aliandika maneno haya kuonyesha kutopendezwa kabisaa na baadhi ya mashabiki walioshadadia kuwa ametundikwa mimba,huku wengine wakionyesha kumnyanyapa.
 
"Imebidi nifute post Ili nielezee upya.Hivi watu hamuelewi kiswahili au ni nini ??? Nimesema tumbo limevimba sababu ya sahani,nikimaanisha mlo na nili post nakula hapo awali Sasa hayo maneno mengine yanatokea wapi? Au niwe naandika kichina? Kwani mliambiwa nitazaa Rais atakaewatoa ktk shida zote mpka mnishikilie mimba mimba
Hebu niacheni basi khaaa Nisiishi Kisa mimba? Aisee mnaboa sana.Basi niueni Kisa sijazaa Ili niwaondolee kero kabisa."
 
Mashabiki wa Lady Jaydee wameonyesha kumtia moyo mwanadada huyo baada ya mashabiki wengine kuanza kuandika vitu vibaya huku wengine wakimzihaki kuwa hawezi kupata ujauzito na kumwita majina ya ajabu ajabu mwanamuziki huyo.
 
"Mwangaza84: Fanya yako mama, binadamu hawakosi la kuongea.Kwani mtu bila mimba maisha hayaendi? Stupid pipo always think about t stupid things.youre the best and you do best music ever in Tanzania hatotokea kama wewe. Big up sisister"
 
"Ilotha_boniphace: "Hayo nimapenzi ya mungu namungu ndio amepanga usijali Jide huyu huyu mungu alie kupa uhai ndo atakupa haja yamoyo wako nahayo nimaneno ya binadamu yanapita but ya mungu kamwe hayapiti so jipe moyo my sister"
 
"Martha_mollel: Hata wao wanavizazi kama wanataka watoto wakazae wao, wakuache, binadam bwana mnaboa mimba mimba si mzae na nyie, mafi yenu..."
 
"Jokofu2: Kila kitu ni majaliwa ya allah kuongelea jambo usilolijua nimpango wa kibinadamu, hivo puuza na usiumize kichwa dada jide."

Comments