Msanii wa kike wa muziki wa kizazi kipya ambaye kwa sasa anafanya vizuri kitaifa na kimataifa Vanessa Mdee amefunguka na kusema kuwa hakupata nafasi ya kuweza kumuuliza Rais Jakaya Kikwete juu ya msimamo wake kwa Wanamuziki Nguza Viking 'Babu Seya' na Papii Kocha wanaotumikia kifungo cha maisha jela.
 
Vanessa alitoa maneno hayo alipokuwa akijibu maswali kupitia kipengele cha Kikaangoni Live wakati aki-chat na watu kwa njia ya facebook ya EATV, ambacho hufanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi alasiri.
 
Vanessa alisema kuwa siku ya hafla ya kumuaga Rais Jakaya Kikwete iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City alipata nafasi japo ya kuweza kuselebuka dansi na rais lakini hakupata nafasi ya kuweza kumuuliza juu ya jambo hilo, hivyo hajui msimamo wake japo yeye binafsi suala hilo huwa linamuumiza.
 
Licha ya swali hipo mashabiki wake walitaka kujua mtazamo wake yeye kama kijana na mustakabali wa taifa lake la Tanzania ndipo hapo Vanessa aliposema kuwa yeye anaamini katika mabadiliko lakini anaamini zaidi kuwa mabadiliko yanaanza na mtu mmoja mmoja kwanza na pia anaamini uongozi bora unahitajika katika kuwezesha mambo mengi zaidi ili vizazi vijavyo viweze kufaidika na rasilimali za taifa.
 
"Napenda mabadiliko ndio but I believe change starts na kila mmoja wetu binafsi kwanza. Naliombea taifa langu kuna mengi bado hatujatimiza na kuna mengi tunaweza kufanya bado, uongozi bora unahitajika utakao wezesha mengi kwa vizazi vijavyo," alisema Vanessa Mdee.
 
Katika hatua nyingine msanii huyo amekanusha taarifa za kutofautiana na msanii Ali Kiba bali anasema anamkubali na kumheshimu sana ingawa anakiri wazi kuwa hawajawahi kufanyakazi ya muziki pamoja lakini anamuamini na anasema kuwa anakipaji cha pekee.
 
"Ali Kiba sina beef naye in fact sina beef na mtu yeyote, nampenda nakumheshimu sana ingawa hatujawahi kufanya kazi ya mziki pamoja lakini ninamuamini sana kwani ana kipaji sanaa na cha kipekee. Tunashirikiana naye kupinga ujangili kama mabalozi wa Wild Aid, " alieleza Vanessa Mdee.
Ukiachia mbali juu ya kazi yake ya muziki watu walitaka kujua mambo mbalimbali kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi na msanii mwenzake wa muziki wa Bongofleva Juma Jux, ambapo aliweza kuweka wazi kuwa mpaka sasa ni mwaka mmoja na miezi minne wapo pamoja kama wapezi na kudai kuwa awali walikuwa washikaji tu na baadae ndiyo walipokuja kuanzisha mahusiano ya mapezi.
 
Kutokana na Comments nyingi kuonyesha kumnyoshea kidole juu ya aina yake ya mavazi na kusema kuwa anavaa nusu uchi, Vanessa Mdee alibidi alifafanue suala hilo kwa kusema kuwa yeye havai nusu uchi bali huwa anavaa nguo za kisanii awapo jukwaani nguo ambazo kwa mtazamo wake ni nguo za kawaida sana kwa msanii kama yeye anapokuwa jukwaani.
 
"Sijawahi kabisa kuvaa nguo inayo onyesha uchi kusema ukweli bali huwa na vaa mavazi ya jukwani ninapokuwa natumbuiza na kuna utofauti,” alijitetea Vanessa Mdee na kuhoji, Je nguo za utamaduni wetu ndio zipi?.
 

.

  • Like Our facebook Page , Follow us on Twitter and Comment on all our posts.
  • Hashtag #pekuatz to share your story with us.
  • Send your post via Whatsapp 0769338868
  • Browse More Posts and Bookmark Our Website for Updates.

Comments