Mwanamuziki  wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed  ‘Shilole’ amepondwa vibaya katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga  Magharibi, Mhe. Kapt. John Komba, baada ya kuvaa kigauni kilichombana na  kumuonyesha maungo yake ya mwili mbele ya viongozi mbalimbali wa  Serikali akiwepo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya  Kikwete.
Mwanamuziki wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiimba pamoja na wasanii wenzake kwenye msiba wa Komba.
 
Baadhi ya watu waliofika katika Viwanja vya Karimjee vilivyopo Posta  jijini Dar, walianza kunong’onezana baada ya mwanamuziki huyo kujitokeza  mbele na kuimba kipande cha shairi lake huku wakisema kuhusu kigauni  alichovaa bi’dada huyo.
 
“ Jamani hii aliyovaa si ‘tight’ kabisa, maana yupo tofauti na wenzake ambao wote wamevaa nguo za heshima zinazowasitiri  maumbo yao, kwa nini yeye ameamua kuvaa hivyo?” alisikika mama mmoja ambaye naye alikuwemo kwenye maombolezo.
 
Mwandishi  wetu alimtafuta Shilole na kumuuliza kuhusiana na hilo alisema hakuvaa vibaya isipokuwa alionekana vile kutokana na umbo la mwili wake.

Comments