Msanii wa bongo movie Batuli ameweka wazi kuwa alikimbia kundi la Kaole sanaa Group baada ya kukutana na changamoto nyingi
 
ikiwepo changamoto ya rushwa ya ngono, Batuli amefunguka hayo leo alipokuwa katika kipengele cha Kikaangoni kinachofanyika kila siku ya Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi Alasiri.
 
Batuli alifunguka na kusema kuwa moja ya sababu kubwa ambayo ilimfanya kuondoka katika kundi hilo ilikuwa kuombwa rushwa ya ngono ili aweze kupewa kipaumbele zaidi kuliko wasanii wengine jambo ambalo kwa upande wake hakuwa tayari kulifanya na kuamua kuondoka katika kundi hilo.
Batuli anasema kabla ya kuweza kutoka kupitia mkono wa Kanumba alishasota sana katika kundi hilo na alikuwa akibaniwa nafasi kutokana na kutokubaliana na watu ambao walikuwa wakimtaka kingono ili waweze kumpa kipaumbele zaidi, ndipo hapo alipoamua kuondoka na baadaye msanii Kanumba ndipo alipoamua kumpa nafasi na kuweza kumtoa kisanaa.
 
"Nilijiunga kaole lakini baadae Kanumba aliniona nafaa kwenye filamu chini ya kampuni ya Game 1st Quality ndivyo nilivyotoka ila kabla ya hapo nilisota sana kwa sababu ya changamoto mbalimbali ikiwepo kubaniwa kazi, na kutakwa kimapenzi au kuombwa rushwa ya ngono moja ya jambo lililofanya niondoke Kaole ni changamoto ya rushwa ya ngono, nilikutana na changamoto hiyo nilipojiunga na kikundi cha kaole nikaamua kuhama kikundi kabisaa"
"Nilijiunga kaole baadae Kanumba alinishika mkono" Aliongeza Batuli
 
Mbali na hilo Batuli alisema kuwa kwa sasa yeye ni mtalaka na ana watoto wawili na katika kipindi chake cha ndoa hakuwahi kuchepuka hata siku moja sababu huwa anapenda kutulia na mtu mmoja, na kuweka wazi kuwa katika maisha yake hajawahi kugombanisha wanaume sababu huwa anapenda kuwa na mtu mmoja anayempenda.
 
"Hapana haijawahi kutokea nimegombanisha wanaume au wanaume wamegombana kwa sababu yangu kwa kuwa huwa sina mahusiano mengi natulia na mmoja"
 
Tunatambua katika tasnia ya filamu na movie nchini wasanii wengi wamekuwa wakitumia kiki na skendo mbalimbali kama njia ya kujitangaza na kujiongezea umaarufu zaidi katika sanaa husika jambo ambalo kwa Batuli limekuwa kinyume chake yeye anaamini kuwa skendo na kiki zinamfanya msanii adharaulike kila na kushusha heshima ya msanii huyo jambo ambalo yeye ameweza lifananisha na vazi baya au chafu katika tasnia ya filamu na sanaa kiujumla.
 
"sio kweli huwezi kuheshimika na kuwa na scandal kuwa na scandals kuna mfanya msanii adharaulike kila aendapo naweza kusema scandals ni vazi baya na chafu kwenye tasnia yetu"
 
WASANII NA SIASA 2015
Batuli ameonyesha kufurahishwa na kitendo cha baadhi ya wasanii kukimbilia katika siasa na kusema kuwa yeye anaona ni jambo zuri kwa kuwa kila binadamu huwa anafuata jambo ambalo yeye mwenyewe anahisi kuliweza kulifanya, hivyo kama wanakwenda huko inamaana wameona wanaweza kuwa wanasiasa wazuri,na kwa mtazamo wake yeye anamiini wataleta mabadiliko kwenye tasnia kwa ujumla.
 
"Naweza kusema kila mtu anafuata kile atakacho au apendacho nadhani wameona wanafaa kuwa kwenye siasa ndiyo maana wanakimbilia huko sasa hivyo hakuna madhara msanii kuamua kuwa mwanasiasa mtazamo wangu ni kuwa wataleta mabadiliko kwenye tasnia kwa ujumla naona wanafaa na wananchi wawape nafasi"
 
Kwa kumalizia Batuli aliwataka vijana wa Tanzania kuzingatia sana elimu kwani elimu ndiyo mkombozi wa kila jambo na wajishughulishe kwa bila kujali kazi au kuchagua kazi
 

"Ushauri kwa vijana wazingatie masomo elimu ndio kila kitu na wajishughulishe bila kujali kazi au kuchagua kazi"

  • Like Our facebook Page , Follow us on Twitter and Comment on all our posts.
  • Hashtag #pekuatz to share your story with us.
  • Send your post via Whatsapp 0769338868
  • Browse More Posts and Bookmark Our Website for Updates.

Comments