Ikiwa ni takribani siku Nne sasa tangu mtanzania, Idris Sultan kuibuka mshind kwenye shindao la Big Brother Africa (BBA ) hotshots 2014, na kunyakua kiasi cha zaidi ya milioni 500. Kama ilivyokuwa kwa watanzania wengi kumuunga mkono kuanzia kwenye kumuombea kura hadi kumpongeza aliposhinda, hali ilikuwa tofauti pale mwanadada  Elizabeth Michael aka Lulu ambe ni muigizaji maarufu wa filamu, alipompongeza  kwakuwepa picha  akiwa na mshiriki huyo na kumpongeza kwa kuandika  “He did it......Idrisssssssssssssss
Proudly Tanzanian".
 
Kitendo hiki kiliwafanya "followers"  wakichukuliae kwa mitazamo tofauti tofauti, Wapo waliona kuwa Lulu amefanya kumpongeza kama walivyofanya watanzania na mastaa wengine,nawengine waliona kama Lulu anataka kujiweka zaidi kwa jamaa wakidai kuwa kwanini asingeweka picha ya Idris pekayake kama walivyofanya watu wengine. Hali ilileta mvutano na kusababisha picha hii kupata comment nyingi zaidi.
 
Hizi ni baadhi ya comeent hizo;
 
#kweli nimeamini mkwanja pekee ndiyo sabuni ya roho, hata kama ulishinda kwenye mashindano ya wenye sura mbaya, ukiupata utakuwa HB.
 
#hii picha alikua nayo toka zamani tangu idris ameingia bba alikua anampa support fyuuuu.....#ndioishakua wivu tu .....mwacheni my qute
 
#Hahaaaaaa achen kutafuta umaaruf knguvu bhana pch wapge wngne nyie mwaleta mkolomo..........
 
#Nini mbaya sasa lulu kupost hiyo pic, watanzania tuamke tuache uvivu wakufikiri, ushindi wa Idris ni ushindi wa Tanzania,acheni wivu jamani, lulu ni mtanzania na ana haki ya kusurport mtanzania mwenzake. Duu jamani,,hongera IDRIS, hongera lulu kwakuona kuwa IDRIS anahitaji pongezi
 
#Tafuta nafasi mkazitumie kwa raha zenyuuuu.
 
#Jmn watu hii pic iliwekwa akiwa anamtangaza kuwa mumpigie kuraa sas bnadam tulivy mnajidai meona leo...wakat ni ya mdaaa
 
#Hahahaa watu km viazi. Hivi kati yenu hapa kama mtu angekuwa amepiga nae picha asingepost.?
 
#Csters mna wivu mpaka shida, mnaona kapata hahhahaha mtaishia kuwa masikin mpaka kufa kwenu vnabo nyie, lulu bibie post unachopenda achana na hawa masikin wa kifikra
 
Idris awewasiri jana kutokea nchini Afrika ya Kusini ambako shindano la BBA lilipofanyikia, akiongea na vyombo vya habari alinukuliwa akisema pesa zake atawekeza kwenye tasnia ya filamu zaidi.
 
Hili nijambo jema kwa  mashabiki na wapenzi na wadau wote wa Filamu hapa Bongo

Comments