MSANII wa vichekesho Bongo, Rashidi Mwinshehe ‘Kingwendu’ amefunguka kwamba japokuwa alipata maumivu ya moyo baada ya jirani yake kumbaka mkewe, Mama Maua ameamua kumsamehe.
 
 Kingwendu alisema mara nyingi mkewe alikuwa Akimwambia kuhusu jirani huyo kumtongoza lakini akawa anamkatalia lakini siku hiyo alimvizia na kutimiza azma yake ambapo baada ya hapo alikimbia mpaka leo hajarudi ila amemsamehe kwa kuwa hata Mungu anasamehe mara nyingi.
 
“Mimi nasali sana hivyo nimeamua kumsamehe huyo jamaa kwa sababu hata Mungu huwa anatusamehe mara nyingi, alishawahi kumtuma dada yake aje kuniomba msamaha maana yeye alikimbilia huko Kilwa na mimi na mke wangu tuko vizuri ninampenda sana na najua halikuwa kusudi lake ila mwanaume huyo alimsumbua kwa muda mrefu,” alisema Kingwendu.

Comments