Maandalizi ya Harusi ya Paul Okoye kutoka P Square pamoja na mpenzi wake Anita Isama, ambayo itafanyika tarehe 22 mwezi huu huko Port Harcourt Nigeria, yameanza kushika kasi ambapo mbali na mambo mengine, zoezi la kusambaza kadi kwa waalikwa maalum wa sherehe hii, tayari limeshaanza.
 
Harusi hii inatarajiwa kuweka rekodi nyingine ya aina yake, na hii ni kutokana na dalili za awali kabisa, ikianziwa na ufahari wa kadi yenyewe ya harusi ambayo tayari imekwishaonekana hadharani.
 
Paul na Anitha waliingia katika uchumba rasmi mwezi Septemba mwaka jana, na tayari wana mtoto mmoja wa kiume ambaye anatambulika kwa jina Andre.

Comments