Kupitia kipindi chake cha 'In My Shoes' kinachorushwa na EATV Wema ameeleza kuwa Kajala hakuwahi kuwa rafiki yake lakini alijitolea kumlipia faini kumuepusha na kifungo. Wema pia alizungumzia kiini cha ugomvi wao ambapo alianika kwamba alichukizwa na suala la Kajala kumsaliti kwa kutembea na mchumba wake aitwaye CK (yule kigogo aliyesumbua mjini kwa kutapanya fedha).

“Kajala hana fadhila, huwezi amini mtu ambaye niliamua kujitolea kwa moyo wangu kumlipia Sh. milioni 13 huyo huyo aje kutembea na mchumba wangu, huku ni kukosa ubinadamu kulikopitiliza,” alisema Wema.

Hapo sasa! Una lipi la kumwambia Wema?

Comments