Msanii kutoka Tanzania House of Talent Msami Giovanni ambaye kwa wakati huu ana hit na ngoma yake ya Sound Track kwa wakati huu inasemekana eti yuko katika dimbwi zito la mahaba na muigizaji maarufu wa 
Bongo Movie Irene Uwoya
,
Gazeti La Makorokocho lilimtafuta Msami na kumuuliza ukweli juu ya Taarifa hizi lakini alichomoa, sikuishia hapo nikamtafuta Girl friend wake wa zamani au niseme ambaye wamegombana kutokana na Msami kuchepukia kwa Uwoya,
Girl Friend huyo anayeitwa Rehema ambaye pia ni Dancer mkali sana maarufu akatiririka kuwa ni kweli taarifa hizo anazo ila ana uhakika Msami atarudi kwake wala hana Wivu na Uwoya na anachofahamu Irene Uwoya eti alimlaghai Msami kwa kumwambia eti anataka kuwa meneja wake kwa kuusimamia muziki wa Msami, sasa tangia hapo wawili hao wakazama kwenye Dimbwi zito la mahaba. 

Comments