Shindano kubwa kabisa la kucheza muziki, Dance 100% 2014 linatarajiwa kuzikonga nyoyo za wapenda burudani kwa mara nyingine siku ya Jumamosi, katika hatua ya nusu fainali ambayo itapambanisha makundi 10 yaliyobakia katika michuano hiyo.
 
Tukio hili litafanyika katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay kuanzia saa 6 mchana ambapo itakuwa ni vita ya ujuzi wa kucheza kugombania nafasi 5 za fainali ya mashindano hayo kwa mwaka huu.
 
Mashindano haya hayana kiingilio ambapo Jumamosi hii swali kubwa la ni makundi gani matano yataaga mashindano haya na ni makundi gani matano yatafanikiwa kusonga hatua ya fainali, litapatiwa majibu.

Comments